Wema Sepetu Ana Nini na Zari ? Tazama Hapa Alichokisema Juu Yake !! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Ana Nini na Zari ? Tazama Hapa Alichokisema Juu Yake !!

Supastaa Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, amefunguka kuwa anachukizwa na watu wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
wema-2
Akizungumza na Za Motomoto News, Wema alisema unatakiwa ufike wakati watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa sasa ni mmoja wa familia hiyo. 
zari-na-aunt
Aunt Ezekiel akiwa na Zari.
“Jamani hebu naomba kwanza wamuache Aunt, hana kosa lolote, hata kama ningekuwa mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni vya kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya kashfa,” alisema Wema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.