Watumiaji wa iPhone Sasa Wataweza Kutuma Ujumbe wa WhatsApp Bila ya Kuwa na Internet - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Watumiaji wa iPhone Sasa Wataweza Kutuma Ujumbe wa WhatsApp Bila ya Kuwa na Internet

Siku za kusubiri uwe internet ili uweze kutuma ujumbe kwenye WhatsApp zinaelekea ukingoni kwa watumiaji wa simu za iPhone.

Feature mpya itawawezesha watumiaji wa simu hizo za kishua (iPhone) kutuma ujumbe wa WhatsApp wakiwa offline. Ujumbe huo utasubirishwa baada ya kuandikwa na kutumwa pindi simu inapopata data. Watumiaji wa simu hizo wanaotaka kutumia feature hiyo wanaweza kufanya hivyo kwa kuweka version mpya WhatsApp (2.17.1) kwenye simu zao.

Kwa watumiaji wa simu za Android wamekuwa wakiweza kufanya hivi tangu kitambo. Watumiaji wa iPhone walikuwa hawawezi kutuma ujumbe bila kuwa na connection. Awali, kitufe cha kutuma kilikuwa hakiwezi kufanya kazi kwenye simu ya iPhone hadi ikiwa na internet.

Hiyo ni update ya kawaida kabisa, lakini yenye umuhimu mkubwa kwa watu wenye mambo mengi. Update hiyo itawawezesha pia watumiaji wa mtandao huo kutuma picha 30 kwa mpigo, tofauti na zamani ambapo waliweza kutuma picha 10 tu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.