Wafaransa Watatu Wasaini Mikataba Mipya Arsenal - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wafaransa Watatu Wasaini Mikataba Mipya Arsenal

Wachezaji wa Arsenal wakati wa kusaini mikataba mipya.


Wachezaji wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francois Coquelin hatimaye wamekubali kuongeza mikataba yao mipya na klabu hiyo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Wachezaji hao wa Kifaransa, beki Koscielny na Giroud wamesaini mikataba hadi 2020, huku mchezaji Coquelin yeye amesaini hadi 2021.

Wafaransa hao wote watatu wamekuwa wachezaji muhimu kwa Arsenal kwa sasa, ambapo Giroud amekuwa gumzo kwa kufunga mabao manne katika michezo minne iliyopita, kujumuisha na bao la kiufundi ‘Scorpion Goal’ alilofunga hivi karibuni kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.