Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Kuigiza Kwenye Tamthilia ya MTV Sugar. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Kuigiza Kwenye Tamthilia ya MTV Sugar.

Vanessa Mdee kwa sasa si muimbaji tu, ameingia kwenye maisha mapya ya uigizaji kwa kishindo.

Mwaka jana alichaguliwa kujiunga kwenye cast ya tamthilia ya MTV Sugar.

Staa huyo ameiambia Bongo5 kuwa tayari wameanza kushoot na huenda Afrika Kusini kila baada ya wiki mbili. Amesema katika maandalizi yake, kila muigizaji hupewa script nzima miezi kabla ya kushoot na baadaye hukutana na kuanza kufanya mazoezi na waigizaji wenzake.Anadai kuwa hulazimika kushika kila kilichoandikwa kwenye script, bila kupunguza ama kuongeza kitu. “Hauongezi wala kupunguza neno lolote na ukiona kama neno haliendani na wewe au huwezi kulikumbuka unaweza kudiscuss na script writers wako on set all the time na kama kuna uwezekano wa kubadilisha wanabadilisha lakini kama haiwezi hakuna,” amesema Vanessa.

Vee amesema kabla ya kuanza kuigiza alikuwa akiogopa sana na sasa baada ya kuona kinachofanyika anawaheshimu zaidi waigizaji.

- Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.