Utata Waibuka Mtoto wa Chuchu na Ray. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Utata Waibuka Mtoto wa Chuchu na Ray.

UTATA mzito umeibuka kuhusiana na mtoto aliyezaliwa na msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans ambapo mashabiki wengi wametaka kujua kama mtoto huyo ni wa Vincent Kigosi ‘Ray’ au nani na kwa nini kuna usiri mkubwa juu ya kuzaliwa kwa mtoto huyo? Ijumaa linakupa hatua kwa hatua.
Ishu ya mimba awali kulikuwa na usiri mkubwa sana kuhusiana na ujauzito wa Chuchu ambapo mara kadhaa alipobanwa na mwandishi wetu alikana kuwa na mimba huku Ray naye akidai hajui lolote kuhusiana na ujauzito wa mpenzi wake huyo.
”Mimi sina ujauzito, watu wanasema tu na kama unataka kuhakikisha, nitakuja hapo ofisini kwenu mnipige picha,” alisema Chuchu lakini kila alipoombwa kuonana na mwandishi wetu alikuwa akichenga. Hata hivyo, kwa kuwa ujauzito haujifichi baadaye ilikuja kubainika kuwa, Chuchu ana mimba kubwa ya kujifungua wakati wowote.
Taarifa za kujifungua siku chache baadaye zilivuja taarifa kuwa, Chuchu kajifungua mtoto wa kiume lakini cha ajabu bado wahusika hao waliendelea kuwa wasiri na hata walipopigiwa simu kuulizwa, walitofautiana kwenye majibu yao.
Msikie Ray mara baada ya Chuchu kudaiwa kujifungua, paparazi wetu alimpigia simu Ray lakini katika hali ya kusha-ngaza, alionesha kutojua lolote.
“Unanipa hongera ya nini? Mimi sina mtoto bwana, hizo habari naziona tu mitandaoni, msinichurie,” alisema Ray.
Chuchu akubali
Wakati Ray akisema hana mtoto, Chuchu alikiri kujifungua mtoto wa kiume huku akim-shukuru Mungu kwa kumzalia mpenzi wake salama.
Madai mazito
Hata hivyo, wakati kukiwa na taarifa tofauti kuhusiana na kujifungua kwa Chuchu, mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alimwaga ubuyu akisema:
“Chuchu kajifungua ila inadaiwa mtoto si wa Ray na ndiyo maana amekuwa mgumu sana kuzungumza. Sura ya mtoto inaonekana haipo kwa Ray wala Chuchu, sasa katika mazingira hayo si unajua mwanaume lazima ustuke.
“Maana unaweza kujishebedua kuwa mpenzi wako kakuzalia mtoto, kumbe si wako. Kwa hiyo ishu ni je, mtoto huyo ni wa Ray au kuna baba mwingne, nadhani Ray akijiridhisha kuwa ni damu yake, atafunguka.”
Kufuatia madai hayo kuwa mtoto si wa Ray, mwandishi wetu alizungumza na Ray tena lakini safari hii alionesha kuna kitu anachokificha kwani alitoa maneno ya kushangaza akisema:
“Mimi watu wananiambia Chuchu kajifungua mbona bado na aliyesema kuwa mimi sijui kama mtoto ni wangu ni nani? Mbona watu wanatunga sana maneno, unajua sio kila mtu anapenda kuweka wazi mambo yake jamani, haya ni maisha yangu, muda wa kuongea ukifika nitasema.”
Chuchu naye ajikoroga
Kuhusiana na madai kuwa, mtoto aliyejifungua si wa Ray, Chuchu alijikoroga katika kutoa maelezo kwani safari hii alikana kujifungua akisema, eti muda huo alipokuwa akiongea na mwandishi wetu alikuwa hospitalini akijisikilizia.
“Kwani Ray alishakana kuwa mtoto si wake? Mbona mimi sijajifungua ndio kwanza nipo hospitali, kuhusu kuficha mimba mwanzo hatukutaka kwa sababu ya mambo binafsi sasa ndio tumeamua kuweka wazi ujauzito na mtoto akipatikana tutaweka wazi. Hapa nipo Muhimbili, natarajia mtoto lakini bado.”
Kuna kitu kinafichwa
Kufuatia utata huo uliopo kuhusiana na mtoto huyo aliyezaliwa, inaonekana wazi kuna kitu kinafichwa ambapo wapo wanaosema labda wanatafuta kiki na wengine kusema huenda ni kweli kuna utata juu ya baba wa mtoto.
Kutoka Ijumaa
Kujifungua kwa mwanamke ni jambo la heri hivyo hakuna sababu ya Chuchu na Ray kuendelea kulifungafunga na badala yake wawe wawazi ili pongezi ziweze kuwamiminikia kwa wakati muafaka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.