Umeyasikia Maneno ya Trump Mara Baada tu ya Kuapishwa Kuwa Rais ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Umeyasikia Maneno ya Trump Mara Baada tu ya Kuapishwa Kuwa Rais ?

Rais Donald Trump wa Marekani ameahidi kuwaunganisha Wamarekani alipokuwa anawahutubia muda mfupi mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.

Trump ameyasema haya.

“Tutaunganisha nchi yetu,”

“Tutaifanya Amerika kuwa taifa kuu tena kwa ajili ya watu wetu wote. Kila mtu, kila mtu, kote nchini. Na hii inajumuisha hata walio mitaa duni.”

“Walisahau kuhusu wengi wetu,”

“Kwenye kampeni, niliwaita mwanamume aliyesahaulika na mwanamke aliyesahaulika. Naam, sasa nyinyi si watu waliosahaulika tena.”

“Mambo yatabadilika, nawaahidi. Mambo yatabadilika.”
Alisema Trump


Trump ameahidi kuilinda miapaka yote ya Marekani huku akieleza kuwa nchi hiyo imekuwa ikifanya juhudi kubwa kulinda mipaka ya nchi nyingine na kusahau mipaka yake hivyo kuingiliwa na wabaya wao na kusababisha maafa makubwa kwa Wamarekani huku akiahidi kufanya mambo ambayo hayajawahi kufanywa nchini Marekani mwa miongo mingi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.