Shilole Amjengea Man Fongo Mjengo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole Amjengea Man Fongo Mjengo.

Mkali wa muziki wa singeli Bongo, Man Fongo amemtaja msanii mwenzake wa bongo fleva na bongo movie, Shilole a.k.a Shishi Trump kuhusika katika ujenzi wa nyumba yake ambayo anataraji kuijenga wakati wowote kutoka sasa.

Man Fongo aliyekuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha Ujenzi cha EATV, amesema mtu pekee aliyemuhamasisha kujenga nyumba ni Shilole, na hiyo ni baada ya siku moja kutembeea nyumbani kwa Shilole na kukuta vitu ambavyo yeye aliona ni vya ajabu na kujikuta anavipenda na kutamani kuwa navyo katika nyumba yake.

Alisema jambo la kwanza alilofanya kukusanya fedha na kununu kiwanja ambacho kiko tayari na amekinunua maeneo ya Kimara Bonyokwa na muda wowote ataanza kuporomosha mjengo wake.

Amesema hawezi kumsahau Shilole kwa kumpa hasira za kuweka mjengo huo, ambao amesema ataujenga taratibu kwa kadri atakavyokuwa anapata pesa na anatamani uwe na vitu vyote vizuri kama ambavyo huwa anaviona kwa washkaji zake hasa Shilole, licha ya kuwa yeye ni mtoto wa uswahilini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.