Roma Afunguka 'Madee Alikuwa Achani Vizuri Ndiyo Maana Akaamua Kuimba' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Roma Afunguka 'Madee Alikuwa Achani Vizuri Ndiyo Maana Akaamua Kuimba'

Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amekana madai ya kuwa kuna baadhi ya wasanii wa hip hop hawafanyi vizuri kutokana na kurap hip hop ngumu.

Rapper huyo amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanafanya hip hop ya aina hiyo lakini anafanya vizuri huku adai msanii kama Madee alikimbia kwenye hip hop na kuhamia kwenye kuimba kwa kuwa alikuwa achani vizuri.

“Kubadilika kwa msanii sio njaa, anajaribu kuwa flexible ili kuonyesha kitu kingine lakini kuna mwingine anahama huku anahamia sehemu nyingine jumla na ipo mifano hiyo, kwani haujawai kumsikia Madee anasema, kwamba hip hop haikuwai kumlipa alivyopiga ‘Pombe Yangu’ mambo yakawa safi. Na mimi nam-challenge, namwambia kwa sababu ulikuwa hauchani vizuri, kwenye kuimba ndiyo umekuja kuimba vizuri,” Roma alikiambia kipindi cha Club101 cha capital Radio.

Aliongeza, “Lakini mimi Roma hip hip ninayoichana inanilipa vizuri kabisa, kwa hiyo kuna wengine wanafanya kitu fulani hawakipatii, wakihama wanaanza kuona mafanikio. Wengine wapatia lakini wanakuwa muda bado, kwa hiyo mimi nawasupport wote cheza na miguu yote, na kubadili ladha ya muziki sio mbaya,”

Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Usimsahau Mchizi’ ambao wameshirikiana na rapper Moni kutoka Dodoma.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.