Professor Jay Afunga Mwaka 2016 Kwa Kumvalisha Pete Mama Watoto Wake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Professor Jay Afunga Mwaka 2016 Kwa Kumvalisha Pete Mama Watoto Wake.

Mbunge wa jimbo la Mikumi, Professor Jay ameitumia vyema siku ya kuuaga mwaka 2016 kwa kumvisha pete ya uchumba mzazi mwenzake Grace Mgonjo zikiwa ni harakati za kuelekea kufunga ndoa.

Mwaka uliopita rapper huyo akiwa katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, aliahidi na kusema kuwa mwaka 2017 atafunga ndoa na mpenzi wake huyo.

Kupitia facebook rapper huyo alipost picha akimvalisha pete mchumba wake huyo na kuandika: Asante sana Mungu, leo (Jana) tunaufunga mwaka namna hii na Mke wa Profjize

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.