Ommy Dimpoz Aikataa Ishu ya Kupangiwa Nyumba, Adai Anajenga Nyumba 2 Dar. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ommy Dimpoz Aikataa Ishu ya Kupangiwa Nyumba, Adai Anajenga Nyumba 2 Dar.

Msanii wa muziki Ommy Dimpoz amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amepangiwa nyumba.

Aidha amedai kwa sasa anaendelea na ujenzi ya nyumba zake mbili, moja ipo Kigambani na nyingine Mbezi.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’ amedai kwa sasa amekodi Apartment Mikocheni.

“Unajua binadamu wanaweza kuongea hiki na hiki lakini ukweli ni kwamba mimi naishi Mikocheni kwenye apartment hivyo siishi Mbezi,” Ommy alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Ila Mbezi kuna sehemu nina site yangu ambayo najenga na site nyingine ipo Kigamboni. Kwa hiyo sina nyumba ambayo nimepangisha au nimepangishiwa kwa hiyo hizo stori sijui bimkubwa sijui nini siyo kweli,”

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai muda haujafika wa kumwonyesha mpenzi wake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.