Nyoshi El Sadaat Ataka Mashabiki wa Muziki Wamkate Miguu, Kisa ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nyoshi El Sadaat Ataka Mashabiki wa Muziki Wamkate Miguu, Kisa ?

Msanii wa band ya FM Academia Nyoshi El Sadaat amesema wanategemea kuachia nyimbo mbili ambazo zimepewa majina 'Nakuita' na 'mama wa Kambo' ambazo ndizo zitakuwa kwa ajili ya mwaka huu 2017.

Akionge kupitia eNEWZ Nyoshi amesema kama media zitatoa sapoti ya kutosha kwa nyimbo hizo na kukosa kufanya vizuri basi mashabiki zake wamkate mikono na miguu ili kuweza kuficha aibu ya uso wake kwa kuwa wamejipanga vizuri na wanahakikisha wanarudisha muziki wa dansi kuwa kwenye chart.

Hata hivyo Nyoshi amesema nyimbo walizoachia kwa mwaka 2016 hazikufanya vizuri kwa kuwa hawakupata sapoti ya kutosha kutoka katika media mbalimbali hali iliyopelekea muziki wa dansi kushuka chart kwa mwaka 2016.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.