Nay wa Mitego Afunguka Juu ya Bifu na Mama Yake Mzazi, Adai Kuwa Hajaongea Naye kwa Miaka 5 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Afunguka Juu ya Bifu na Mama Yake Mzazi, Adai Kuwa Hajaongea Naye kwa Miaka 5

Nay wa Mitego amefunguka kuwa aliwahi kukaa miaka mitano bila ya kuongea na mama yake mzazi.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Sijiwezi’ amekiambia kipindi cha Planet Bongo Cha EA Radio Ijumaa hii kuwa kitendo hicho kilitokana na mazingira ya mtaani aliyokuwa anaishi lakini kwa sasa anaishi pamoja na mama yake na wako poa kabisa.

“Mimi na mama mzazi tuko poa sana na nina kaa naye this time. Ni kweli kabisa tumekaa miaka mitano bila kuzungumza jambo lolote lile, ila ni mazingira ya maisha ya mtaa niliyokuwa naishi lakini mpaka muda huu tunaongea mimi naishi na mama yangu nyumbani kwangu, hivyo niko naye nyumbani.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.