Manchester United Kuikabili Saint Fainali ya EFL. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Manchester United Kuikabili Saint Fainali ya EFL.

Wachezaji wa Man United wakishangilia goli la kusawazisha

Mashetani wekundu wa Man united wametinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la ligi Elf licha ya kuchapwa kwa mabao 2-1 na Hull city.

katika mchezo nusu fainali ya kwanza united walishinda kwa magoli 2-0 hivyo wamesonga mbele ya jumla ya mabao 3-2.

Kiungo wa Hull City Tom Huddlestone alianza kuindikia timu yake bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 35 ya mchezo.

Manchester United walichomoa bao hilo katika dakika ya 66 kipindi cha pili kupitia kwa kiungo wake Paul Pogba.

Katika dakika ya 85 Baye Oumar Niasse akaipatia timu yake ya goli la pili na la ushindi lakini licha ya ushindi huo Hull hawakuweza kufuzu hatua ya fainali baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Man United watachuana na Southampton katika fainali itakayopigwa kwenye dimba la Wembley Jijini London hapo Februari 26.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.