Man United Ndio Klabu Yenye Pesa Ndefu Zaidi Duniani, Ona Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man United Ndio Klabu Yenye Pesa Ndefu Zaidi Duniani, Ona Hapa

Hii ni kwa mara ya kwanza Man U kuongoza tokea mwaka 2004

Timu ya Manchester United imepata kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita kulingana na taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi duniani (Deloitte).

Manchester United imewashinda Real Madrid waliofanya vizuri katika michezo kwa miaka 11baaada ya kukusanya kipato kikubwa takribani Euro 689 katika msimu wa 2015-2016.

Clubu za ligi ya Premier imeshuhudia kukua kwa kipato kwa Euro Millioni mia moja.
Mauzo makubwa ya jezi ni moja ya chanzo cha mapato kwa United

Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4 hii haijawahi kutokea.

Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushikilia nafasi hiyo tokea msimu wa 2003-04.
Barcelona inasalia nafasi ya pili

Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Barcelona katika nafasi ya pili.
Madrid imeshuka mpaka nafasi ya tatu

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wapo nafasi ya nne huku matajiri wa jiji la Manchester Man City wakiwa nafasi ya tano kwa kutengeneza Euro milioni 524 kwa msimu uliopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa Man city kuingia katika nafasi hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.