Liverpool Kumsafirisha Mane kwa Ndege ya Binafsi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Liverpool Kumsafirisha Mane kwa Ndege ya Binafsi.

Sadio Mane ameifungua Livepool mabao 8 msimu huu

Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya kibinafsi mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kushiriki mechi na viongozi wa Ligi Chelsea.

Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakai wa mechi za robo fainali siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.

Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushirika mechi za kimataifa.

Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.