Kuhusu Young Dee na Meneja Wake Max Rioba, Muda Utatuambia Ukweli ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kuhusu Young Dee na Meneja Wake Max Rioba, Muda Utatuambia Ukweli !

Ukweli na muda ni ndugu, tena ndugu haswa waloshibana. Muda haujawahi kuacha ukweli upite bila kujulikana – inaweza kufika kipindi ukahisi pengine muda na ukweli vimetengana lakini pale inapobidi ukweli kudhihirika muda huacha ukweli udhihirike.


Miezi michache iliyopita rapa Young Dee pamoja na meneja wake Max Rioba waliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwa kile walichokiita Young Dee kuomba radhi kwa kujiingiza kwenye madawa ya kulevya na kuahidi kurudi katika hali ya kawaida na kufanya muziki.

Ilikua habari nzuri kwa mashabiki wa Young Dee na watanzania kwa ujumla kuona Young Dee amesanuka kabla mambo hayajaenda kombo zaidi. Lakini habari ni kuwa Max yule aloenda naye kwenye vyombo vya habari amenukuliwa akisema eti Young Dee amerudia kutumia, ngada!

Yananijia mambo mengi kichwani, mosi; inaweza kuwa Max anamchukia Young Dee,lakini amchukie kwa kwa sababu gani? Kwa lipi analolipata kwa yeye kumchukia? Au pengine kuna watu wanampelekea Max maneno yasiyo ya kweli? Yes hili ni jibu sahihi kwangu nahisi. Pengine naweza kuonekana mwendawazimu kwa kuamini eti kuna watu wasiompenda Young Dee wanamharibia kwa Max, kwa kumpelekea uzushi na maneno yasiyo ya kweli

Kwanini naamini hivyo? Kwa sababu sitaki kuamini Young Dee ameamua kucheza na akili za watanzania kuwaambia ameacha kutumia Ngada halafu eti miezi michache mbele arudie kule?! Sitaki kuamini kuwa ni kweli kwa sababu siamini Young Dee haoni jinsi ambavyo wasanii wanaotajwa kutumia madawa wanavyodhalilika na kudhihakiwa kwenye mitandao ya kijamii. Naamini vipi kijana alotoka kuitwa baba juzi tu hapa akasahau kuwa ana jukumu la kumlea mwanaye na kujitumbukiza kwenye madawa siamini kama youngdee anaweza akasahau hilo!

Lakini kama alivyo sema yeye Young Dee, “time will tell” ngoja tusubiri na tuone,japo sitamani muda unapokuja kutuambia ukweli awe kwenye hali mbaya. Sitamani kuona ukweli ukiniacha nikijiona mwendawazimu kwa kumwamini Young Dee kiasi hicho. Lakini angalizo ndugu yangu kama yanayosemwa ni kweli usiogope kuupokea ukweli mchungu,mwanadamu anapoendelea kuvuta pumzi anakuWa ana nafasi zisizo na idadi za kujisahihisha. Umri na wakati bado ni rafiki kwako unaweza ukajisahihisha bila hata Dongo Janja kujua kuwa ulikosea. Kazi kwako Daudi.

By Eliezer Gibson ”greencitynative

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.