Kuhusu Ishu ya Madee ya Kupora Simu, Sasa Sikia Alivyojitetea Juu ya Tukio Hilo ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kuhusu Ishu ya Madee ya Kupora Simu, Sasa Sikia Alivyojitetea Juu ya Tukio Hilo !

Msanii wa bongo fleva Madee amesema hajutii matusi yanayotukanwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa amepora simu kwa kuwa wanaomtukana hawaujui ukweli na wakiujua watatulia.

Akionge kupitia eNewz Madee amesema hajapora simu bali alikuwa anadai pesa ambayo aliitoa kwa
ajili ya kufanyiwa kazi na badala yake haikufanyika jambo lililomfanya aende kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kurudishiwa pesa yake, na ndipo hayo yakatokea.

"Baada ya kuona pesa yangu ipo tu imekaa hafanyi kazi yoyote, nikafuatailia sheria, nikaenda polisi, nikasaidiwa kupata haki yangu, nashukuru nimepata haki yangu, wala sijutii kinachoendelea, sasa mi naweza kupora simu rafiki yangu, mi natumia simu yangi iPhone 7 na hiyo simu nayoambiwa nimepora ni S4, halafu kama ni kupora nisingeenda na polisi" amefafanua Madee

Pia Madee amesema pesa yake huwa haipotei hata kama ikiwa imechukuliwa na maiti.

Hata hivyo Madee amesema uongo huwa hauishi muda mrefu hivyo hawalaumu wale ambao wamemtukana kwa kuwa hawaujui ukweli na anaamini kuna siku watu wote wataujua ukweli.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.