Joh Makini Atoboa Siri Kubwa ya Kundi la ‘Weusi’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Joh Makini Atoboa Siri Kubwa ya Kundi la ‘Weusi’

Rappa kutoka kundi la Weusi Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ameamua kutoa siri ya kundi hilo ambalo pengine kwa watu wengine walikua hawajui sababu ya kundi hilo kuendelea kudumu mpaka leo wakati baadhi ya makundi mengi yameshindwa kuendelea.

Weusi ni muungano wa makundi mawili ambayo ni River Camp Soldiers pamoja na Nako 2 Nako Soldiers makundi hayo yalikua yanatokea Arusha Tanzania,ndipo wakakaa na kukubaliana kuunganisha nguvu na kutengeneza kundi la Weusi lililozaa Kampuni kwa sasa,mmoja kati ya memba wa kundi hilo Joh Makini ametoa sababu ya wao kuendelea kusimama pamoja mpaka leo.

Kwenye mahojiano yake na Clouds FM Rappa huyo amesema >>’Nimshukuru tu Mungu kwa sababu vitu hivi mara nyingi hutokea mara chache sisi mbali na muziki tulikua marafiki zamani,kabla hatujawa kundi tulikuwa solo kabla ya kukubaliana kuanzisha Weusi kampuni,inamaana sisi ni watu tuliokuwa tunaishi pamoja tu ingawa kila mmoja alikua akishughulika na brand yake’

‘Kikubwa ni kuheshimiana,kupendana na kuwa wazi pamoja na kutoingiliana kwenye maamuzi binafsi ya mtu,siku zote unaona tunapush mtu mmoja mmoja kwa sababu hatutaki mtu awe tegemezi kwenye kundi’

‘Watu wanapokuwa tegemezi ndiyo baadae huleta maneno tunaamini katika ushirikiano wetu jinsi tunavyoshirikiana kutengeneza brand ya mtu mmoja mmoja inatufanya tupende kuendelea kuwa pamoja kwa sababu siku zote umoja ni nguvu’

‘Sisi ni zaidi ya marafiki,familia na kiukweli Weusi kampuni inatusaidia sana kama msanii mmoja mmoja na kama kundi pia’

Kundi la Weusi lina vichwa vitano ambavyo ni Joh Makini, G Nako, Nikki wa Pili na Bonta.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.