Ivory Coast Yavuliwa Ubingwa AFCON. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ivory Coast Yavuliwa Ubingwa AFCON.

Wachezaji wa Moroco wakishangilia.

Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya afrika tembo wa Africa Ivory Coast, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 na Simba wa Atlas Moroco

Goli pekee liliowaondoa miamba hao wa soka wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.

Nayo timu ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ilitambia Togo kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara kwa kundi C kwa alama 7 huku Moroco wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.