Hiki ni Kitu cha Kujifunza Kwenye Mapenzi ya Jux na Vanessa Mdee. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hiki ni Kitu cha Kujifunza Kwenye Mapenzi ya Jux na Vanessa Mdee.

Inawezekana wewe ni mmoja kati ya watu ambao wanaovutiwa na mapenzi ya Jux na Vanessa Mdee labda kwa namna wanavyoishi,kwa namna wanavyopendana hata kwa namna ambayo wao wanaendesha maisha yao ya kimuziki na mapenzi.

Jux amesema kuwa maisha wanayoishi ni yale ya kila mmoja kupambana kadri anavyoweza >> ’Unaweza kuwa na mpenzi wako,yaani wote wawili jaribuni kusaidiana usiwe mzigo kwa mwenzako kwa namna alivyo,na kuishi kwa kuamini kwa sababu yeye ni msichana alitakiwa kuamka asubuhi akuandalie chai,hata kama kachoka’
‘Unaweza kuamka mapema mpenzi wako akiwa kalala we ukatengeneza chai ukamuamsha aje kula,huwezi kusema kwa sababu wewe ni mwanaume huwezi kufanya hivyo, kikubwa mwanaume atabaki kuwa mwanaume na mwanamke atabaki kuwa mwanamke lakini wote muwe mnafanya kitu kwa sababu yenu na sisi ndiyo tunavyoishi hivyo’ Jux.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.