Fid Q Ataja Tarehe ya Kutoka Kwa Album Yake ya ‘Kitaaolojia’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fid Q Ataja Tarehe ya Kutoka Kwa Album Yake ya ‘Kitaaolojia’

Ni mwaka wa tatu sasa tumekuwa tukisubiri album ya tatu ya Fid Q, Kitaaolojia.

Kwanini haitoki, ama nayo inataka kuwa kama Detox ya Dr Dre? Habari njema ni kuwa, album hiyo mwaka huu lazima iingie mtaani ili kusambaza hiyo elimu ya mtaa, iliyobeba jina lake.

“Kitaaolojia ni kweli ina miaka mitatu imekuwa kama Detox na nini, lakini unajua mimi ni perfectionist, natakaa itokee kweli konki,” Fareed ameiambia Bongo5.

“Na idea zimekuwa zikibadilika mara kwa mara, lakini so far sasa hivi nimeshaipatia direction, na kuna uhakika ninaweza nikawaguarantee kabisa kwamba August 13 ya mwaka huu panapo majaliwa Kitaalojia itakuwa mtaani,” amesisitiza.

Fid ameshatoa album mbili hadi sasa, Vina Mwanzo Kati na Mwisho na Propaganda.

-Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.