Drogba Kuhamia Klabu ya Brazil - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Drogba Kuhamia Klabu ya Brazil

Didier Drogba

Mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba, 38, yuko katika mazungumzo ya kuhamia klabu ya Brazil ya Corinthians Paulista, gazeti la Jeune Afrique limeripoti.

Drogba hajahusishwa na klabu yoyote tangu mwezi Disemba alipoiaga klabu ya Impact de Montreal ya Canada.

Kwa hivi sasa ana matarajio ya kujiunga na klabu ya Corinthians Paulista kwa msimu wa 2017.

Raia huyo kutoka Ivory Coast alitaka kurudi Olympique de Marseille ambapo alipata umaarufu msimu wa 2003-2004, lakini kocha Rudi Garcia hakuunga mkono pendekezo hilo, Gazeti hilo la Paris limeripoti.

Gazeti hilo la Jeune Afrique limemukuu Drogba akisema: ''Kwa hivi sasa, mazungumzo yamekuwa yakiendelea kuhusiana na klabu ya Brazil ya Corithians kwa mkataba wa miezi sita hadi 12." Drogba amekuwa akisubiri majibu ambayo yanaonekana kuwa mazuri'.

Drogba alitangaza kustaafu kwake kutoka kwa soka ya kimataifa miaka miwili iliyopita.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alifunga magoli 65 katika mechi 104 alizoshiriki timu ya taifa Ivory Coast kwa miaka 12.

Amechezea michuano ya kombe la kimataifa mara tatu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.