Diamond Awakomesha Alikiba na Wema Instagram. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Awakomesha Alikiba na Wema Instagram.


MREMBO asiyeishiwa matukio kila kukicha Bongo, Wema Isaac Sepetu na msanii wa Bongo Fleva anayewika kwa wimbo wake Aje, Ali Kiba, mwisho wa wiki hii wamenagukia pua katika mitandao ya kijamii na Diamond Platnumz ameendelea kuwaonyesha kuwa yeye ana nguvu kuwazidi wao mtandaoni.

Awali iliripotiwa kuwa Wema amefuta picha zake zote katika mtandao wake wa Instagram kwa shabaha ya kurudi kwa kishindo na kuwaonyesha watu kuwa yeye ndiye malkia wa mtandao huo hapa nchini. Jitihada zake ziligonga mwamba pale aliporejea na kutegemea mapokezi makubwa na haikuwa hivyo. Daimond aliweka video ya familia yake iliyowaonyesha laivu akiwa na mkewe na mwanaye Tiffa Dangote.

Video hiyo ilipata watazamaji 20,708 na wachangiaji zaidi ya 600 na kusababisha watu wengi kuacha kumzingatia Wema na kurudi kwa Diamond. 

Aidha Ali Kiba amekuwa akiendelea kushushiwa matusi na kupewa lawama na mashabiki zake baada ya kuonekana mahojioano kupitia vituo mbalimbali vya televisheni akisema kuwa yeye hapo alipofika ni juhudi zake.

Mashabiki zake hawakupendezwa na kauli hiyo na kuitafsiri kama majigambo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.