Chris Brown Amwomba Radhi Karrueche. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chris Brown Amwomba Radhi Karrueche.

Mkali wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumwomba radhi mpenzi wake wa zamani, Karrueche Tran.

Uhusiano wa wawili hao ulivunjika tangu Machi 2015, baada ya msanii huyo kuletewa mtoto wa miezi tisa ambaye alimpa jina la Royalty, mtoto huyo alimpata na mrembo mwingine ambaye alijulikana kwa jina la Nia Guzmann.

Tangu Chris aachane na mrembo huyo, amedaiwa kutoka na mwanamitindo Krista Santiago, lakini cha kushangaza msanii huyo amemwomba radhi Karrueche.

“Nilikuzoea, tulikuwa wote sehemu mbalimbali, naomba tuyasahau hayo,” aliandika msanii huyo baada ya kuiposti picha ya mrembo huyo.

Hata hivyo, maneno ya msanii huyo yanadaiwa kumweka katika wakati mgumu kwa mpenzi wake wa sasa, Krista.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.