Baruti na Moshi Kwenye Video Hizi Mpya za Bongo Zina Maana Gani ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baruti na Moshi Kwenye Video Hizi Mpya za Bongo Zina Maana Gani ?

Nafurahi ninapoona video kali zinazofanya vizuri kwenye channel za Bongo na nje ya Bongo ambazo zimeongozwa na director wazawa pia.


Kuna kipindi waongozaji walikuwa wanalalamika kuwa wasanii wanakimbilia nje kushuti video, wakati hata wao wakipewa bajeti nzuri wanaweza kufanya kazi nzuri.

Naweza kuwapongeza wasanii kwa kuona hilo licha ya kuwa bado serikali inalalamikiwa kuwa haitoi sapoti ipasavyo. Lakini kwa video hizi zilizotoka mwezi huu tena kwa kufukuzana pamoja na kuwa ni video kali ila naona kuna kitu kinajirudia tena kisicho na maana yeyote.

Kama utakua umeitaza video ya ngoma ya Roma na Moni, ‘Usimsahau Mchizi’ utakuwa umeona bidada mmoja akichezea baruti za moshi fulani hivi. Hivyo hivyo pia kwenye video ya Madee ‘Hela’ tunaona tena jamaa akichezea zile baruti za moshi.

Video ya tatu ni video ya Bill Nas ft Mwana FA kimejitokeza tena kitendo cha kuchezea baruti za moshi kwamba ni kuishiwa idea au?

Nilikuwa natazama Clouds TV nikaona video zote zimechezwa tena kwa mfululizo kama nilivyozielezea nikaona kama directors kwa hili mmefeli.

Kesho na kesho kutwa mtakimbiwa kutokana na kukosa ubunifu mdogo tu japo mnatupa video zenye quality nzuri hatakama baruti ndio zinaingia nchini sidhani kama lazima kwenye kila video zitumike vingine tuwaachie maharusi.

Nafananisha mkumbo huu kama kipindi drones zimeingia mjini. Kila muongozaji alitaka tu kuweka shot ya drone hata kama hakukuwa na ulazima, ili kuonesha tu kuwa ‘nami ninayo na ninaweza kuitumia drone.’ Nadhani ni vyema waongozaji wakawa wanaweka vitu kwenye video kwa lengo lenye maana, na si kama fashion tu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.