Bahati Bukuku Adai Hana Mpango wa Kuolewa Kwa Sababu Hii Hapa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bahati Bukuku Adai Hana Mpango wa Kuolewa Kwa Sababu Hii Hapa.

Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku amefunguka na kuweka wazi kuwa ndoa ilimshinda na kusema katika harakati za maisha yeye alipishana na aliyekuwa mume wake kufikia hatua ya kutengana na sasa kila mmoja kuishi kivyake. 


Bahati Bukuku akizungumza kwenye  cha Kikaangoni alisema wimbo wake wa 'Dunia haina huruma' si kama alimwimbia huyo aliyekuwa mume wake bali anakiri kuwa ni kisa cha kweli kilichotokea lakini hayo mambo aliyekuwa mumewe alikuwa hayafanyi.

"Aliyewahi kuwa mume wangu hakufanya hilo tukio ila kile kisa ni kweli kilitokea sehemu, lakini aliyekuwa mume wangu hakuwa na matatizo haya, ila tu katika harakati zetu za maisha kuna kupishana hivyo nilipishana naye tu. Siwezi kuongea uongo kwa mtu aliyekuwa mume wangu, hata nikiandika kitabu siwezi kuruka hili popote nikisimama nitasema niliolewa ndoa ikanishinda" alisema Bahati Bukuku 

Baadhi ya mashabiki walitaka kujua endapo alipata watoto katika ndoa hiyo, ambapo Bahati alikataa kuongea chochote kuhusu yeye kuwa na watot au la, na kusema kuwa hayuko tayari kuongea chochote huku akisema kuwa ana watoto wengi

"Hili swala la watoto sitaki kuzungumzia, mimi nina watoto wengi tu, kwahiyo kwenye ndoa yangu nisingependa kuongelea swala la watoto" alisema Bahati

Mbali na hilo Bahati Bukuku anasema watu ambao walimzushia kifo ni watu wake wa karibu ambao anafanya nao kazi na huenda walifanya hivyo ili kutaka kumpunguzia mashabiki wake.

"Walionizushia kifo ni watu ambao nafanya nao kazi, walidhani watanipunguzia mashabiki lakini pia ni kazi ya shetani hiyo, hivyo walijifanya ile taarifa imeanzia Congo lakini ni wa hapahapa ila mamlaka za mawasiliano bado zinaendelea kufuatilia ingawa mpaka sasa tayari wameshafahamika" alisema Bahati Bukuku 

Katika hatua nyingine, Bahati amesema hivi sasa anaandaa movie ambayo pia itakuwa na lengo la kuinjilisha, na kufikisha ujumbe wa Mungu kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye uimbaji.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.