AY Afunguka Kuhusu Collabo Yake na Busta Rhymes. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

AY Afunguka Kuhusu Collabo Yake na Busta Rhymes.

Tutarajie collabo kati ya AY na Busta Rhymes mwaka huu kwani kwa mujibu wa rapper huyo mkongwe, meneja wake wa Marekani Hemdee ndiye anayeweka mipango sawa ya kufanyika kwa wimbo huo.

“Hemdee bado anaendelea kuishughulikia hiyo kazi na mwaka huu tunaweza kuwa na rekodi moja na Busta Rhymes,” AY amemuiambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

“Bado hatujaanza kurekodi lakini bado tunaendelea kuumiza kichwa tujue beat ni ya aina gani, tufanyaje sisi na yeye,” ameongeza AY.

Rapper huyo ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kwanza kufanya collobo na wasanii wa Marekani akiwemo Romeo, L’amyia na Sean Kingston.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.