Albamu Mpya ya AIM ya Navy Kenzo Haikamatiki Mitandaoni. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Albamu Mpya ya AIM ya Navy Kenzo Haikamatiki Mitandaoni.

Ikiwa ni baada ya Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili kutoka Bongo, Aika na Nahreel kuachia Albamu yao mpya ‘Above In A Minute (AIM)’ kwenye mfumo wa CD, album hiyo sasa imeingia kwenye mitandao kwa fujo, kwani mashabiki walimiss kupata albamu nzima kutoka kwa wasanii baaa ya soko kubadilika miaka ya nyuma na wasanii kuwa wanaachia wimbo mmoja mmoja.

Kinachoendelea kwa sasa ni kwamba, mashabiki wanaweza kuipata album hiyo kupitia iTunes, Spotify, Tidal, Akazoo na Boom Player. Kupitia Boom Player unaweza kustream bure kabisa. Hii ni mara ya kwanza kwa album ya Tanzania kuingia mtandaoni kwa uzito huo.

Tangu itoke, AIM imepokea maoni chanya zaidi na kutajwa kuwa miongoni mwa album bora za Afrika kwa sasa. Kwenye album hiyo wasanii walioshirikishwa ni pamoja na Alikiba, Patoranking, R2Bees, Mr Eazi na Rosa Ree.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.