Vanessa Mdee Apata Shavu La Kuigiza MTV Base Kwenye 'Shuga' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vanessa Mdee Apata Shavu La Kuigiza MTV Base Kwenye 'Shuga'

Baada ya kumaliza mwaka na wimbo wa ‘Cashmadame’, mkali wa muziki Afrika Mashariki, Vanessa Mdee, mwakani ataanza kuonekana kwenye tamthilia ya Shuga iliyochezwa nchini Afrika Kusini.

Msimu wa tano wa tamthilia hiyo unaanza Machi mwakani ambapo Vanessa Mdee kutoka Tanzania atashirikiana na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali katika kunogesha msimu huo wa tamthilia hiyo.

“Nafurahi mwaka huu naumaliza vizuri na wimbo wangu wa ‘Cashmadame’ lakini mwakani Mungu akipenda nitauanza tena vyema kwa kuwa nimechaguliwa na MTV Base nishiriki katika tamthilia ya Shuga kwa msimu wa tano, ni mafanikio makubwa kwangu na kwa taifa langu na hii ndiyo itakuwa tamthilia yangu ya kwanza kuwahi kuigiza,” alieleza Vanessa.

Tamthilia hiyo anayokwenda kushiriki Vanessa ina umaarufu mkubwa kutokana na watu wengi maarufu kuwahi kushiriki, akiwamo mshindi wa tuzo ya Oscar mwaka 2014, Lupita Nyong’o kupitia filamu ya‘Twelve Years a Slave’.

Unafahamu Kuwa Tupo Instagram ? >Bofya Hapa< Kuungana Nasi Upate Uhondo Zaidi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.