Tunda Man: ‘Debe Tupu’ Sio Dongo Kwa Diamond Platnumz, Watu Wanashindwa Kuelewa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tunda Man: ‘Debe Tupu’ Sio Dongo Kwa Diamond Platnumz, Watu Wanashindwa Kuelewa.

Tunda Man amefunguka kuwa cover la wimbo wake mpya ‘Debe Tupu’ halijamlenga mtu yeyote.

Kumekuwepo na maneno mengi yaliyozuka mitaani kuwa muimbaji huyo amemdiss hitmaker wa Salome kupitia cover ya wimbo wake huo inayomuonyesha paka akijitazama kwenye kioo na kujiona kama Simba.

Tunda amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio one, “Kitu kikubwa watu wanaangalia ile cover kwa jicho la tatu, waangalie kwa jicho la kawaida tu. Mimi paka niliyemzungumzia ni yule yule paka wa nyumbani na simba niliyemzungumzia ni yule yule wa Mikumi. Mtu anatoa zile tafsida nionekane nimemsema vibaya, kwa hiyo wachukulie kawaida Tunda amemweka yule paka wa jikoni na Simba yule wa Mikumi wala sijamzungumzia mtu na debe tupu ni mwanamke au anaweza akawa ni mwanaume.”

Tunda ameongeza kuwa aliamua kutoachia wimbo wake wa ‘Mwanaume Suruali’ baada ya Mwana FA kumpigia simu na kumtaka asiachie kwa sasa wimbo huo kwa kuwa na yeye alikuwa anataka kuachia wimbo wake ‘Dume Suruali’ ili wasiwachanganye mashabiki.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.