Rose Muhando Akanusha Kutumia Madawa ya Kulevya ‘Situmii Madawa na Sitatumia’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rose Muhando Akanusha Kutumia Madawa ya Kulevya ‘Situmii Madawa na Sitatumia’

Msanii mkongwe wa nyimbo za Injili nchini Rose Muhando amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa ameingia katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Muimbaji huyo alidai taarifa hizo zilisambazwa na watu ambao hawamtakii mema katika maisha yake kutokana na kwenda nao tofauti katika makubaliano ya kufanya nao kazi.

“Situmii madawa na sitatumia, kama waliona ndiyo skendo itakayonimaliza wameshindwa, wanaofanya hivyo ni watu wanaotaka kunimaliza walitaka nifanye kazi zao, nikakataa.” Rose aliuambiia mtandao wa gazeti la Mwanaspoti.

Aliongeza, “Sijajiingiza na mambo hayo na wanavyozungumza nasikitika kwa sababu wanaiumiza familia yangu kisaikolojia, mimi ni mama wa watoto watatu na nina ndugu zangu, naambiwa mambo yote hayo kwa sababu sina mtu wa kunitetea,”

Katika katua nyingine muimbaji huyo alizungumzia kuhusu ukimya wake pamoja na ujio wake mpya.

“Nipo hata hivyo kuna kazi nyingine nimeandaa ipo kwa Alex Msama bado haijatoka kutokana na mambo mbalimbali, ingawa naandaa kazi nyingine ninayotegemea kuikamilisha mwezi wa tatu mwakani tutakapojaaliwa. Nimeshaanza kuandaa baadhi ya nyimbo na nyingine naendelea kutunga, unajua kazi hizi huwa nasikiliza sauti ya Mungu aniambie niimbe nini.”

“Pia, nimekuwa nafanya huduma ya kuimba katika mikutano tofauti ndani na nje ya nchi kama hivi jana umenikuta natoka kijiji cha jirani kuimba na wiki iliyopita, nilikuwa Kenya ambako nilifanya huduma, Kisumu na Mombasa, nimeamua kufanya hivyo kwa sababu zangu,” anasema Rose.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.