Klabu ya Arsenal Imepost Ujumbe Kuhusu Uhuru wa Tanzania Bara. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Klabu ya Arsenal Imepost Ujumbe Kuhusu Uhuru wa Tanzania Bara.

Wakati Tanzania bara ikisherekea miaka 55 tangu ipate uhuru wake, klabu ya Arsenal inayocheza ligi kuu ya England imepost picha kwenye mtandao wa Facebook ya bendera ya Tanzania iliyoandikwa ‘Happy Independence Day Tanzania.’

Si jambo dogo kwa klabu kubwa kama Arsenal kuonesha kutambua siku hii muhimu ya kitaifa kwa Tanzania ambayo huadhimishwa kila mwaka, sherehe za maadhimisho ya Uhuru zimefanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli.

Arsenal pia inamashabiki wengi nchini na huenda taarifa hii ikawa njema zaidi kwao kwa kuona ni namna gani klabu wanayoipenda imeguswa na tukio muhimu katika taifa lao.


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.