Huu Ndio Muonekano wa Zari The Bosslady Baada ya Kujifungua, Utapenda Hii. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huu Ndio Muonekano wa Zari The Bosslady Baada ya Kujifungua, Utapenda Hii.

Zari The Bosslady amerudi barabarani siku chache tu baada ya kujifungua mtoto wake wa pili na Diamond.

Akiwa kwenye makazi mapya – kwenye nyumba yao na mchumba wake supastaa iliyopoto Pretoria, SA, mama huyo mwenye watoto watano kwa ujumla, hakutaka kuchelewa kurejea kwenye maisha yake ya kupendeza.

Amepost picha tatu Instagram ambapo ya kwanza akiwa kwenye gari ameandika: When mummy got some errands to run.”
Nyingine anayoonekana akiwa amempakata mtoto huyo wa kiume anayedaiwa kupewa jina ‘Riaz’ (kinyume cha jina Zari), ameandika: Simply do what suits your lifestyle and health in general.”
Nyingine ameonekana akiwa amesimama kwenye mlango wa nyumba yao iliyonunuliwa kwa takriban shilingi milioni 400.

Pamoja na Riaz, Zari na Diamond ni wazazi wa mtoto maarufu zaidi kwenye Instagram barani Afrika, Tiffah.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.