Hizi Ni Mbinu 13 za Kufanikiwa Kifedha Ambazo Rafiki Yako Tajiri Hatakwambia⁠⁠⁠⁠. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi Ni Mbinu 13 za Kufanikiwa Kifedha Ambazo Rafiki Yako Tajiri Hatakwambia⁠⁠⁠⁠.

Kila siku panapokucha kila mmoja huianza mihangaiko ya siku akitarajia kuwa kile anachokifanya kitamwezesha kufanikiwa na siku moja ataishi maisha ambayo anayatamani.

Watu wengi wakiwa katika mihangaiko hiyo kuna mtu ambaye tayari amefanikiwa (role models) huwa wanamuangalia wakitamani kufanikiwa kama yeye au hata zaidi yake. Wakati mwingine watu hawa hutumia muda wao na wale wanaowaiga ili waweze kuwaambia ni njia gani walizoweza kuzitumia wakafanikiwa na kufika hapo walipo.

Lakini watu husema huwezi ukamuuzia adui ramani ya vita. Japo hapa si suala la uadui lakini usitegee akwambie kila kitu. Ukweli ni kuwa kuna mambo ambayo hatokwambia ili aweze kujihakikishia kuwa anapunguza ushindani. Hapa chini ni orodha ya mbinu 13 za kufanikiwa kifedha ambazo rafiki yako tajiri hatakwambia.

1. Anatumia kidogo kuliko anachopata. Anaweka akiba zaidi. Anafahamu ni bora kuwa tajiri usiyejulikana kuliko kuwa masikini na kuishi kwa kujifanya tajiri.

2. Anajua kwamba uvumilivu unalipa. Lakini uvumilivu bila juhudi hauna maana. Ukifanya kazi leo ukitarajia kesho uwe bilionea utakuwa hauishi katika uhalisia. Mafanikio ni zao la muda.

3. Ukienda kwake utakuta chai, mlo kamili na vitu muhimu mezani. Huwezi kukuta kanunua kitu ambacho hakina faida kwa mwili zaidi ya matatizo.

4. Hapendi madeni na akiwa nayo anayalipa. Hanunui kitu kwa mkopo bila sababu ya msingi. Anafahamu kwamba Kama kitu huwezi kukulipia cash basi huna uwezo nacho na ni budi ukajipanga upya.

5. Anafahamu kwamba uhuru wa kifedha ni jambo la nafsi. Uhuru wa kifedha maana yake kuishi bila deni na sio kuwa na fedha lukuki na madeni lukuki wakati huo huo.

6. Anafahamu kwamba kuwa na shughuli mbili za kufanya sio tu kwamba kunakuongezea kipato lakini pia kunakunyima muda wa kutumia fedha vibaya kwa kukuweka ‘bize’.

7. Anafahamu Pesa ni kama mtoto mdogo, haiwezi kujisimamia na kujiongoza yenyewe, lazima uisimamie wewe mwenyewe.

8. Anafahamu kwamba utajiri wa kweli mara nyingi unakuja unapofanya kitu unachokipenda.

9. Anajua ukishindwa kuwa na mipango maana yake unajikosesha mafanikio tayari.

10. Haishi kwa kuwaza kushindwa. Anafahamu mwanzo wa mafanikio ni kujiamini.

11. Anajua kwamba muda sio rafiki wa binadamu. Kwa hiyo anaheshimu muda kwa kiwango cha juu kabisa.

12. Anafahamu kwamba huwezi kutumia usicho nacho. Hawazi kuanza kutumia fedha kabla hajaifanyia kazi. Haishi katika ndoto anaishi katika uhalisia.

13. Anakushangaa kwamba unaendesha gari ya milioni 14, mkeo gari ya milioni 12, na wote ofisini zenu ziko karibu karibu, na magari yote ya mkopo na umepanga nyumba vya vyumba 5 wakati una mke na watoto wawili tu.

USIONDOKE KWENYE POST HII BILA KU SHARE NA MARAFIKI ZAKO JAPO WA 5 TU ILI UKOMBOE MAISHA YAO.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.