Guardiola Ataka Wachezaji wa Ziada Kuongezwa, Adai Wachezaji Wana Haki ya Kupumua. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Guardiola Ataka Wachezaji wa Ziada Kuongezwa, Adai Wachezaji Wana Haki ya Kupumua.

Kocha Pep Guardiola wa Manchester City ataka idadi ya wachezaji wa ziada kuongezwa hadi sita.

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa Fifa inafaa kufikiria kuongeza wachezaji wa ziada na kufikia hadi sita ili kukabiliana na tishio la kuwachosha wachezaji.

Shirika la soka duniani Fifa wiki hii lilithibitisha kuwa litaongeza idadi ya timu zinazoshiriki katika kombe la dunia hadi 48 ikiwa na makundi 16 yenye timu tatu.

Guardiola amesema kwa hatua ya kuongeza idadi ya mechi zitakazochezwa itawachokesha wachezaji.

''Wanafikiria kuongeza idadi ya mechi, kwa kweli kutaathiri ubora'', alisema raia huyo wa Uhispania .

''Nazungumza kwa niaba ya wachezaji. Wana haki ya kupumua, na kupumzika ili kufurahia.Wanaongia kwa sasa ni wachezaji watatu pekee, kwa nini isiwe wanne,watano ama hata sita''.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.