Diamond Platnumz: Bob Junior Amenisaidia Sana Kwenye Muziki Wangu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platnumz: Bob Junior Amenisaidia Sana Kwenye Muziki Wangu.

Hivi uliwahi kufikiria kuwa licha ya kutemana katika kazi lakini Diamond Platnumz bado anathamini mchango na uwezo mkubwa wa Bob Junior.
Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz kinacho hostiwa na Salama Jabri, Diamond alieleza mambo muhimu aliyofanyiwa na Bob Junior katika harakati zake za Muziki.
Bongoswaggz inakupa maneno ya moyoni jinsi Diamond Platnumz anavyojivunia kwa kuanza kufanya kazi na Bob junior

Kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika katika maisha yangu kwa sababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeza. Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kama anaweza kuwa producer mzuri sana. Lakini mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye, nakufa naye mimi yaani huyu natoa nyimbo na inahit,” aliongeza.

Kuna mengi yamemkuta pia Chibu lakini hakusita kusema pia harakati alizopitia kwenye maisha yake ya mziki.


“Nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita, Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Binadamu, nyimbo tofauti tofauti. Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana. Na mpaka nakumbuka ilifika time niliweka kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu fulani, yeye akasema mimi ni producer, natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali, akasema huyu nikimpa analeta beat kali.”Alisema Diamond.

Tiffah wa Diamond Akiwa na Gari Yake Aina Ya Bentley. Tazama hapa chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.