Darassa Ajiwekea Rekodi Mpya Kwenye Muziki Wake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Darassa Ajiwekea Rekodi Mpya Kwenye Muziki Wake.

Uamuzi wa kubadilisha muziki wake, umeendelea kumzalia matunda matamu rapper Darassa. Akiwa na wimbo ambao hakuna anayeweza kubisha kuwa ndio namba moja nchini kwa sasa, Muziki, mkali huyo kajiandikia rekodi yake nyingine katika CV yake.

Video ya wimbo wake huo imefikisha zaidi ya views milioni 1 ndani ya wiki mbili tangu iwekwe kwenye mtandao wa Youtube. Ni nadra sana kwa msanii anayerap kufikisha idadi hiyo ya views katika kipindi hicho.

Wimbo huo kwa muda mfupi umemfanya Darassa awe miongoni mwa wasanii wanaotafutwa sana kwa show wakati huu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.