Darassa Aendelea Kufanya Vizuri na 'Muziki' Sasa Yapaa Kimataifa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Darassa Aendelea Kufanya Vizuri na 'Muziki' Sasa Yapaa Kimataifa.

Kama ni mwaka wa historia ambao unaweza ukaandikwa na rapper Darassa basi huwenda mwaka 2016 ukaandikwa kwa kalamu nyekundu katika kitabu cha kumbukumbu cha rapper huyo.

‘Acha maneno weka muziki’ hiki ni kipande pendwa kinacho wapagawisha wapenzi na mashabiki wa Darassa katika nyimbo yake ya ‘Muziki’, na tayari nyimbo hiyo aliyo shirikishwa Ben Pol imeanza kuvuka mipaka ya Tanzania baada ya kutunyoosha takribani miezi kadhaa tangu kuachiwa kwake.

Kituo cha Trace Africa kutoka Ufaransa kimeucheza mwimbo wa Darassa aliyomshirikisha Ben Pol na kuupa nafasi ya kwanza kama nyimbo bora ya HipHop.

Wasanii wengi wa bongo wameanza kuona matunda ya kazi zao baada ya kuanza kukubaliwa na vituo vikubwa vya kimataifa, ikiwa ni ishara nzuri kuwa muziki wa kibongo bongo sasa umeanza kuota mabawa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.