Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo ya Ballon d'Or 2016. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo ya Ballon d'Or 2016.

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa sasa wameshinda tuzo hii wakipokezana kwa miaka tisa mfululizo.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.

Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.

Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.
Lionel Messi alishinda tuzo hii 2015

Kwa sasa ameshinda Ballon d'Or 2008, 2013, 2014 na 2016 na tokea mwaka 2009 amekuwa akipokezana na Messi.

''sikuwahi kuwaza kama ningeshinda Ballon d'Or mara nne'' nina furaha kubwa sana, najisikia fahari'' alisema Ronaldo.

''Natumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji wenzangu, timu yangu ya taifa, makocha na watru wote walionisaidia kupata tuzo hii.''
Ronaldo ametaja mwaka 2016 kama bora kwake.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amefunga magoli 19 katika michezo 20 kwa klabu na timu ya taifa msimu huu.

Orodha ya wachezaji bora wa dunia tokea mwaka 2003.

2016: Cristiano Ronaldo

2015: Lionel Messi

2014: Cristiano Ronaldo

2013: Cristiano Ronaldo

2012: Lionel Messi

2011: Lionel Messi

2010: Lionel Messi

2009: Lionel Messi

2008: Cristiano Ronaldo

2007: Kaka

2006: Fabio Cannavaro

2005: Ronaldinho

2004: Andriy Shevchenko

2003: Pavel Nedved

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.