Baraka Da Prince Atangaza Music Label Yake, Itamsimamia Pia Lord Eyez na Naj. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baraka Da Prince Atangaza Music Label Yake, Itamsimamia Pia Lord Eyez na Naj.

Kwenye muziki, mdogo wako wa leo, anaweza kuwa bosi wako wa kesho. Kuanzia sasa, rapper mkongwe wa Nako 2 Nako na aliyekuwa mmoja wa members wa kundi la Weusi, Lord Eyez atakuwa chini ya usimamizi wa label mpya mjini – BANA, inayomilikiwa na Barakah The Prince.

Barakah ameitangaza label yake hiyo Jumanne hii wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa TV. Muimbaji huyo wa Nisamehe amedai kuwa Lord Eyez ataungana na mpenzi wake, Naj kama wasanii wa label hiyo na kwamba hivi karibuni nyimbo zao zitatoka.
Amedai kuwa lengo la kumchukua Lord Eyez ni kutokana na kukubali uwezo wake na kwamba kutokana na kutumbuiza naye kwenye show kadhaa, amegundua kuwa ana mashabiki kibao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.