Baada ya Rihanna na Rick Ross, Diamond Ana Collabo na Jay Z ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Rihanna na Rick Ross, Diamond Ana Collabo na Jay Z ?

Well, well, this one is big! Baada ya yeye mwenyewe pamoja na meneja wake Sallam kuthibitisha kuwa kuna collabo ya Diamond pamoja na mega superstars wa Marekani, Rihanna na Rick Ross, hitmaker huyo wa Salome ametease kuwepo kwa nyingine na samaki mkubwa zaidi kwenye bahari ya muziki wa Marekani.

Akiongea hivi karibuni na mtangazaji wa Clouds FM B-Dozen kwenye show yake ya Beach Party Jangwani Sea Breeze, Diamond alisema, “[Kitu] ambacho sijakifanya, ni kutoshoot nyimbo yangu na Jay Z, yawezekana ikawa ni tatizo hilo pia labda,” alisema na kusababisha shangwe kutoka kwa watu wengi waliokuwa wakisikiliza mahojiano hayo.

Dozen alimuuliza,” Unataka kusemaje, kwamba una collabo na Jay Z?”
“Ahh Dozen tuishie hapo,” alijibu Chibu kwa kicheko. Kabla ya Dozen kumalizia,” halafu huyu hapa anatuachaga hivi hivi kila siku yaani.”

Kama asemacho Diamond kina ukweli wowote, hiyo inaweza kuwa silaha nyingine ya kuringishia katika career yake, sababu Jigga si mtu wa mchezo mchezo kumpata kirahisi kwa collabo, hata Wamarekani wenzake kumshirikisha ni bahati!

DJ Khaled na ukubwa wake wote, alitumia mwaka mzima ili kumpata kwaajili ya kumshirikisha kwenye album yake ya mwaka huu, Major Key.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.