Aunty Ezekiel: Siwezi Tena 'Ku-Kiss' Kwenye Filamu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Aunty Ezekiel: Siwezi Tena 'Ku-Kiss' Kwenye Filamu.

Star wa Bongo Movie nchini mwanadada Aunty Ezekiel, amerudi upya kwenye tasnia hiyo huku akiweka wazi baadhi ya mabadiliko aliyoyafanya katika maisha yake kuwa ni pamoja na kutoweza tena 'ku-kiss' kwenye movie atakazocheza.

Aunty ambaye kwa sasa amerejea na movie mpya inayokwenda kwa jina la Chritmass Eve, amesema kilichomfanya afikie maamuzi hayo ni majukumu aliyonayo kwa sasa ya kifamilia ikiwa ni pamoja na malezi ya mtoto.

Akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV Aunty amesema kuanzia sasa akiwa kwenye movie, kabla hajakubali ku-kiss na mtu kwanza anamkumbuka mtoto wake huku akitaja mabadiliko mengine kuwa ni kuweza kuigiza kama 'house girl' uhusika ambao awali aliwahi kusema hawezi kuuigiza.

"Nimechenji baada ya kuzaa, nimekuwa na mawazo tofauti, nimerudi nyuma mara mbili hata ikitokea kwenye movie natakiwa ku-kiss, najifikiria sana hivi mwanangu akiona atafikiria nini" Alisema

Amesema hivi sasa amebadilika kwa kuwa amekuwa mtu mzima na kusisitiza kuwa kwa sasa ameacha mabo yote ya kitoto aliyokuwa akiyafanya ikiwemo kuishi kwa skendo maana ameona hayana faida.

Katika hatua nyingine Aunt alisema anatarajia kupata mtoto wa pili ambaye angependa awe wa kike.

-eatv

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.