Alichosema Samatta Baada Jina Lake Kutajwa Kwenye Wimbo wa Darassa na Mavoko. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alichosema Samatta Baada Jina Lake Kutajwa Kwenye Wimbo wa Darassa na Mavoko.

Baada ya jina lake kutajwa kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Flavor, mshambuliaji wa kibongo anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji amesema kwake ni heshima kubwa kuwepo kwenye nyimbo za wasanii na inaonesha ni namna gani wanavyothamini kitu anachofanya.

Star huyo wa soka la Tanzania ametajwa kwenye nyimbo mpya za Darasa (Muziki) na Rich Mavoko (Kokoro) ambazo kwa sasa zinafanya vizuri kwenye soko la muziki.

“Wasanii wakubwa kama hao wanapokuzungumzia na kukutaja kwenye nyimbo zao ni jambo la kujivunia, ni suala zuri na nimejisikia poa. Nimejisikia faraja yani moyo wangu umekuwa baridi, kumbe kuna kitu nafanya wanakipenda kwa hiyo fresh kabisa,” amesema Samatta amabye ame-assist goli moja lililofungwa na Heynen katika mchezo wa Europa League dhidi ya Sassuolo uliomalizika kwa Genk kupata ushindi wa magoli 2-0 ugenini.

“Yani hizo ndio ngoma zangu kwa sasahivi zilizonishika kwa kiasi kikubwa, nasikiliza muda mwingi hata nikiwa naenda kwenye game nasikiliza nazisikiliza hizo ngoma.”


Tiffah wa Diamond Akiwa na Gari Yake Aina Ya Bentley. Itazame Hapa Chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.