Video: Aliyeitusi 'Chibu Perfume' Instagram WCB Yampa Chamtema Kuni. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Aliyeitusi 'Chibu Perfume' Instagram WCB Yampa Chamtema Kuni.

Instagram ni miongoni mwa mitandao pendwa zaid duniani.lakini kwa hapa bongo mtandao wa instagram unatumiwa kama nyumba ya udaku, mipasho, matusi, na mambo ya team kadhaa za baadhi ya wasanii.

Leo inatimia siku ya 4 tangu kutambulishwa kwa bidhaa mpya ya 'chibuperfume' lakini siku ya jana anapatikana mtu alikuwa akiwapa maneno machafu baadhi ya wasanii na wasiokuwa wasanii pia kwa kuwatusi. Dhuruba limemkuta mmiliki huyo wa account ya shilolekiuno_official.
Uongozi wa WCB Wasafi umeonyeshwa kuchoshwa na tabia hiyo na kuamua kulivamia swala hilo na kuhakikisha amepatikana na sheria inafuata mkondo yake.

Meneja wa Diamond Salam SK ametumia ukurasa wake wa Instagram na kutupa ujumbe huu kuhusu mtu huyo.

“Kwa watu wote kama ulitukanwa na huyu ambae anaejiita @shilolekiuno_official kwa sasa yupo chini ya mikono ya sheria, Kama una mashitaka yoyote fika Oyster Bay Polisi, Vizuri ametaja watu wanaemtuma afanye hivyo! Na kuwasaidia wale ambao wanajiamini kuwa hawawezi kujulikana basi kwa taarifa yenu Serikali ina mkono mrefu sana! Eti Jana alikuwa anamuita Diamond “Simba” ???.”

ITAZAME VIDEO HAPA BIGWA WA MATUSI ALIVYO KUTANA NA SERIKALI.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.