TID Muziki Halisi wa Bongo Fleva Umepotea Kabisa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

TID Muziki Halisi wa Bongo Fleva Umepotea Kabisa.

Msanii mkongwe kwenye game ya muziki wa bongo TID aliewahi kupata skendo mbalimbali hapa bongo lakini leo kaja na kitu tofauti hasa alipokuwa akifanyiwa mahojianao na EFM Alhamisi hii, TID amesema muziki wa bongofleva umetokana na mchanganyiko wa muziki wa hip hop na RnB.

“Uhalisia ya muziki wa bongofleva umepotea watu sasa hivi wanataka kuimba kama Wanigeria, watu wanataka kuiga vitu vya nje lakini wakumbuke kwamba bongofleva maana yake ni mchanganyiko wa muziki wa hip hop na RnB,” alisema TID.
Muimbaji huyo amesema aliamua kuandika wimbo ‘confidence’ ili kuwaonyesha vijana wanatakiwa kufanya nini kwenye nyimbo zao.
BongoSwaggz inakupa nukuu ya TID aliyoizungumza kwenye mahojiano :
“Ni mara chache sana kwenye tuzo zetu kushuhudia tuzo za heshima zinatoka kwa ‘legends’ wa muziki wetu kutambua mchango wao, hata aliyeanzisha tuzo za muziki za Kilimanjaro marehemu James Dandu sijashuhudia akipewa heshima yake tuzo hizi zinapofanyika.” alisema TID.

Diamond Platnumz Anakuletea Perfume Yake Inaitwa 'Chibu Perfume' Itazame Hapa Chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.