Serikali Yaitaka Sekta Binafsi Kuwekeza Katika Kinywaji Aina ya Gongo Ili Kurasimisha Kinywaji Hicho. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Serikali Yaitaka Sekta Binafsi Kuwekeza Katika Kinywaji Aina ya Gongo Ili Kurasimisha Kinywaji Hicho.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezishauri kampuni zinazotengeneza vilevi kutengeneza pombe yenye ladha ya gongo, kwa kuwa baadhi ya wateja wanavutiwa na ladha hiyo wana wanakipenda kinywaji hicho.

Mwijage ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Gimbi Masaba (Chadema) aliyehoji mpango wa serikali wa kuanzisha na kuhalalisha viwanda vya kutengeneza pombe aina ya gongo ili kuchochea uchumi wa nchi na kubainisha kuwa, gongo ikitengenezwa kiwandani itafuata ubora unaotakiwa kisheria.

“Moja ya kigezo muhimu cha kuanzisha kiwanda ni uwepo wa soko, kutokana na wananchi kupenda kinywaji hiki(gongo) nawashauri wadau wa sekta hii kuwasiliana na ofisi za Sido ambazo zinapatikana mikoa yote ili kupata muongozo juu ya uanzishaji wa viwanda bora na salama vya aina hii,” alisema Mwijage.

Amesema haiwezekani Serikali kuhalalisha gongo, ila inaishauri sekta binafsi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi zinazotengeneza kinywaji hicho kwa lengo la kuzalisha kinywaji kinachokidhi viwango vya usalama na ubora wa chakula.

Katika swali la nyongeza, Masaba amehoji kama serikali ipo tayari kufanya utafiti kujua faida zilizo kwenye gongo.

Mwijage amesema faida zinafahamika, lakini atawaelekeza wataalamu wake waendele maeneo yenye gongo na pombe nyingine za kienyeji ili kuzifanyia utafiti na zitengenezwe kwa kufuata ubora na viwango.

- mpekuzihuru

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.