Ratiba ya Mazishi ya Spika Mstaafu, Samwel John Sitta Ipo Hapa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ratiba ya Mazishi ya Spika Mstaafu, Samwel John Sitta Ipo Hapa.

Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta aliyekuwa Spika wa Tano wa Bunge la Tanzania utawasili nchini Tanzania kutoka Ujerumani siku ya Alhamisi jioni na utahifadhiwa nyumbani Masaki, Dar es Salaam.

Siku ya Ijumaa saa 3 asubuhi mwili wa marehemu utaagwa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam katika ibada itakayoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa na Mchungaji Mwaipole wa KKKT Kinondoni.

Baada ya ibada hiyo, saa 6 kamili mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Dodoma kwa ndege na saa 8 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine watauaga kabla ya kusafirishwa kwenda Tabora saa kumi jioni.

Mazishi ya Marehemu Samwel John Sitta yatafanyika siku ya Jumamosi Urambo mkoani Tabora.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.