Picha 5 za Kusisimua za Trump na Obama Walipokutana. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha 5 za Kusisimua za Trump na Obama Walipokutana.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump alipokutana na Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza ikulu ya White House tangu ashinde uchaguzi, uadui kati yao ulijidhihirisha.

Bw Trump kwenye kampeni alimweleza Bw Obama kama rais mbaya zaidi kuwahi kuongoza Marekani.

Rais Obama naye alisema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.

Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na alikejeliwa hadharani na Rais Obama.

Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu kuficha uadui kati yao.

Waliongea maneno mazuri kuhusu umoja na umuhimu wa kupokezana madaraka kwa amani.

Lakini picha zilizopigwa zinaonesha jambo tofauti, ukiangalia sura na mikono...
Fikira za Trump zinaonekana kuyumba ... labda kwa kukumbuka aibu iliyotokana na utani kuhusu kuzaliwa kwa Obama mwaka 2011.
Wanasalimiana lakini macho yako wapi.... taama mdomo wa Trump
Tena, sasa Obama anamwangalia Trump.... lakini Trump anaamua, la hasha, SIWEZI kumwangalia machoni
Kupeana mikono kwisha sasa, na ni furaha sana kwa Trump .... lakini anaonekana kutoyaamini anayoyasema Rais Obama


Lakini yote hayakuwa kununa tu...
Wawili hao walicheka wakati mmoja walipotaniana.

Melania na Michelle pia walikutana, lakini hawakuonekana kuwa na matatizo.


Melania Trump na Michelle Obama wakiwa ikulu ya White House

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.