Ommy Dimpoz: Wema Sepetu Hajawahi Kuwa Mpenzi Wangu Hata Kidogo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ommy Dimpoz: Wema Sepetu Hajawahi Kuwa Mpenzi Wangu Hata Kidogo.

Ilikuwa ni kwenye The Playlist ya Times Fm ambapo Ommy Dimpoz alikuwa kama mgeni wa kipindi hicho na kama ilivyo kawaida kuulizwa maswali kibao kuhusu kazi yake ya muziki na hata maisha yake ya kila siku.

Moja kati ya maswali ambayo Lil Ommy alimuuliza Ommy Dimpoz ni pamoja na mapicha picha ambayo yalimake headlines ya yeye na Wema Sepetu kipindi cha kuiachia video ya wimbo wa Wanjera, na Lil Ommy alitaka kujua kuwa kuna chochote kilichokuwa kinaendelea baina ya wawili hao.


“No, watu walisahau kama Wema ni actress na ana uhuru wa kufanya chochote. Na katika ufanyaji wa kazi kama ile ni lazima kuwe na majaribio kama yale, haikuwa kitu cha serious. Ila ni mshkaji wangu, nampenda kwasababu siku zote amekuwa akinisapoti na mimi pia nasapoti kazi zake lakini hatuna mahusiano ya kimapenzi.” alisema Ommy Dimpoz.

ITAZAME HAPA VIDEO YA OMMY DIMPOZ ANAVYOMKANA WEMA SEPETU.
TAZAMA HAPA DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOTUONYESHA CHIBU PERFUME.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.