Ommy Dimpoz: Kukaa Kimya Kwenye Muziki Sio Kupotea Kimuziki. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ommy Dimpoz: Kukaa Kimya Kwenye Muziki Sio Kupotea Kimuziki.

Muimbaji Ommy Dimpoz amesema ukimya wake kwenye muziki sio kwamba alipotea bali alikuwa anafanya mambo mengine nje ya muziki.

Ommy Dimpoz amesema watanzania wamekuwa na mtazamo tofauti sana hasa pale msanii anapokuwa kimya kwenye kazi zake, na kukimbilia kumlaumu.

“Mimi nilikuwa kimya nilikuwa nafanya mambo yangu mengine, lakini sio kama kukaa kwangu kimya nilikuwa nimepotea kwenye muziki,” Ommy aliiambia FNL ya EATV. “Unajua watanzania wamekuwa na tafsiri tofauti, kuna watu wanatake break akina Justin Timberlake wanakaa miaka 7, na mimi nilikuwa zangu vacation, ma Ibiza huko, sasa nimerudi nataka kufanya kazi”,

Muimbaji huyo amerudi na wimbo Kajiandae akiwa ameshirikiana na AliKiba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.